Mourinho akata kiu ya mashabiki wa Manchester United Ligi ya Mabingwa

Kikosi cha Jose Mourinho kimetoa dozi nzito baada ya kuilaza CSKA Moscow kwa mabao 4-1, huku akiacha kilio kwa mashabiki wa klabu hiyo ya Urusi wakiwa nyumbani kwao.
Mpaka kipindi cha kwanza Manchester United ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyowekwa wavuni na wakali wa mabao Romelu Lukaku (2), Anthony pamoja na Henrikh Mkhitaryan.
Mshambuliaji Lukaku huo ni mchezo wake wa saba akiziona nyavu za wapinzani tangu atue kwenye dimba la Old Trafford msimu uliopita wa usajili wa kiangazi katika jumla ya mechi 9 alizocheza huku akifunga jumla ya mabao 10.
Mourinho akata kiu ya mashabiki wa Manchester United Ligi ya Mabingwa Mourinho akata kiu ya mashabiki wa Manchester United Ligi ya Mabingwa Reviewed by EXUPER ASSOCIATION on 03:36 Rating: 5

Post Comments

Powered by Blogger.