
Manchester United inapanga kumnunua Antoinne Griezman kwa kitita cha £88m kutoka Atletico Madrid msimu ujao baada ya mkufunzi Jose Mourinho kuomba uhamisho huo kukamilishwa (Daily Express)
Chelsea wanatumai kwamba kiungo wa kati Eden Hazard, 26,ataweka kandarasi ya mkataba mpya ambao utamfanya raia huyo wa Ubelgiji kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi ya Uingereza kwa £300,000 kwa wiki. (Sun)

PSG itaipiku Manchester City katika kumsajili Alexis Sanchez kwa kumpatia mchezaji huyo wa Arsenal £9m kabla ya kumsajili mnamo mwezi Januari. (El Mecurio, via Sun)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa huenda akamsajili mchezaji mwengine wakati wa dirisha la uhamisho mnamo mwezi Januari ili kuchukua mahali pake Benjamin Mendy , 23, ambaye anauguza jeraha la goti.(Independent)
Manchester United na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomsaka mshambuliaji kinda wa MK Dons' Dylan Asonganyi. (Daily Mirror)

Real Madrid iko tayari kushindana na wapinzani wao Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Juventus' Paulo Dybala, 23. (Mundo Deportivo, via Daily Star)
Chelsea wanapigiwa upato kumsajili Edinson Cavani iwapo mshambuliaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 30 ataondoka PSG mnamo mwezi Januari. (Sun)
Winga Antonio Candreva anatarajiwa kuondoka Inter Milan, huku Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte akivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.(Calciomercato, via Daily Star)
Everton huenda ikawasilisha ombi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Kevin Gameiro ,30, ambaye huenda asicheze mara kwa mara kufuatia kuwasili kwa Diego Costa katika klabu hiyo. (Daily Mirror)

Liverpool na Tottenham wameungana na Arsenal pamoja na Real Madrid katika kumwania winga wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 19. (TransferMarketWeb via Daily Star)
Kiungo wa kati wa West Brom Gareth Barry alipatiwa jezi ya Arsenal iliosaniwa na Arsene Wenger baada ya The Gunners kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya The Baggies, ili kumtambua kwa kuvunja rekodi ya Ryan Giggs ya kushiriki mechi 632 katika ligi ya Uingereza. (Daily Mirror)

"Karibu nyumbani kwangu karibu London .Ahsante kwa kututembelea'' -kiungo wa kati wa Arsenal Ozil alichapisha katika mtandao wake wa Instagram na kuwapatia watazamaji kuangalia kila eneo la nyumba yake ambapo alionyesha jezi nyingi za mazoezi , magari na kioo cha kutazama filamu.
Wachezaji wa Anderlecht watalipwa marupurupu ya £35,000 kila mtu iwapo wataishinda Celtic katika mechi ya Jumatano ya vilabu bingwa dhidi ya Celtic mjini Brussels (Daily Record)
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville amekiri kwamba alifurahishwa wakati mchezaji mwenza David Becham alipoondoka Old Trafford mwaka 2003 kuelekea Real Madrid. (Manchester Evening News)
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 28.09.2017
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
21:35
Rating: