Nyambui kwa sasa anafundisha riadha katika timu ya Taifa ya Brunei, alisema kelele za klabu hizo zimezidi uwezo wa mastaa wao ambao wanawasajili kwa mbwembwe.
"Niwe wazi mimi ni mpenzi wa Yanga, ila kipindi kile cha wachezaji kina Sunday Manara ama Abdallah Kibaden wa Simba siyo hiki na ukumbuke wale walicheza kwa mapenzi na siyo sasa wanavyomwagiwa pesa lakini bado hawakati kiu ya wadau wapenda soka,"anasema.
Anasema ifikie hatua kila Mtanzania kwenye sekta anayofanyika kazi, awajibike ipasavyo kwa lengo la kuleta maendeleo ya taifa.
"Waonyeshe kwamba wanahitaji mabadiliko ndipo kutatokea hatua ya maendeleo lasivyo kama watendaji wanapenda njia za mkato inakuwa hatari ya kuwa na maendeleo,"anasema.
Nyambui atupa dongo kumwaga fedha za usajili lakini uwanjani sifuri
Reviewed by EXUPER ASSOCIATION
on
21:05
Rating: